Photo Gallery

  • UFATILIAJI WA MAENDELEO YA MRADI WA KUBORESHA HUDUMA Y MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MOROGORO ( AFD).

    Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mha. Mwajuma Waziri amewataka Wataalam Washauri wa Mradi wa Kuboresha Huduma ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (AFD) kuhakikisha wanafanya kazi inayoonekana kwa macho ''Site'' katika utekelezaji wa Mradi huo.

    .

    Wmetoa maagizo hayo Leo Novemba 21, 2023 wakati wa kikao cha Ufuatiliaji wa Maendeleo ya Mradi huo wenye thamani ya Tsh. Bilioni 185 na kusisitiza kuwa utekelezaji wa Mradi huo upo nyuma ya muda na hawana budi kuhakikisha wanaongeza kasi.Katika maagizo yake pia amewataka Wataalam Washauri wa Mradi huo kukamilisha nyaraka za zabuni ifikapo Disemba 2023.

    Pia amewasisitiza kufanya kazi kwa ushirikiano na kushirikisha wadau ili kuleta tija na matukio mazuri katika utekelezaji wa Mradi huo.

    aye Mkurugenzi Mtendaji, Mha. Tamim Katakweba amesema kuwa watajitahidi kuhakikisha maelekezo ya Naibu Katibu Mkuu yanatekelezwa ili Mradi uweze kukamilika kwa wakati.

    Kikao hicho kimeenda sambamba na ziara ya kutembelea baadhi ya maeneo yanayohusika katika utekelezaji wa Mradi huo ambayo ni Bwawa la Mindu, eneo la kujenga Mtambo mpya wa kutibu maji Mafiga na Mabwawa ya Kutibu Majitaka Mafisa.

    Posted On : september, 25,2023

  • BODI YA MORUWASA YAZINDULIWA RASMI.

    Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso amezindua Bodi 25 za Mamlaka za Maji nchini ikiwemo MORUWASA na kuzitaka bodi hizo na viongozi wa sekta ya Maji kuhakikisha zinatoka huduma za Maji za uhakika sambamba na kuzingatia utoaji wa taarifa kwa wananchi.

    .

    Waziri Aweso amesema hayo wakati akifungua kikao cha mafunzo ya siku mbili kwa Wakurugenzi wa bodi na Menejimenti za Mamlaka za maji, jijini Dar es salaam.

    Aidha, amewasisitiza kushirikiana na kujenga mahusiano mazuri na wadau na sekta zingine ili kuleta tija katika utoaji wa huduma za maji.

    ilevile Mhe. Aweso amesisitiza kuhusu kuwekwa kwa mkakati wa kukabiliana na upotevu wa Maji yasiyolipiwa (NRW) kwani haikubaliki suala hilo halipaswi kuzoeleka na kuwa jambo la kawaida.

    Pia amewataka kushughulikia changamoto na kero za watumishi na wateja kwa wakati.

    Kikao hicho kimeenda sambamba na upandishaji wa madaraja wa Mamlaka mbalimbali za Maji nchini kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa ikiwa ni pamoja na upana wa mtandao na kumudu gharama za uendeshaji.

    Posted On : september, 25,2023

  • MTAALAMU MSHAURI WA MRADI WA MAJI MOROGORO ASISITIZWA KUKAMILISHA KAZI YA USANIFU KWA WAKATI .

    Mkurungezi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) Mha. Tamim Katakweba amemtaka Mtaalam Mshauri kampuni ya Egis Water and Martime ya nchini Ufaransa akishirikiana na kampuni ya Ice Project Service Ltd ya nchini Tanzania kukamilisha taarifa ya mwisho ya usanifu wa Mradi wa Uboreshaji huduma ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro kwa wakati.

    .

    Mha. Katakweba ameyasema hayo leo Septemba 13, 2023 wakati wa kikao na wataalam washauri hao katika ofisi za MORUWASA, Morogoro Mjini.

    Pia amesisitiza wataalamu washauri hao kuzingatia ubora na kuhakikisha hadi kufikia Desemba 2023 kazi ya usanifu wa mradi iwe imekamilika ili kuwezesha upatikanaji wa Mkandarasi wa ujenzi wa mradi na kuanza kazi rasmi ya ujenzi ifikapo mwanzoni mwa mwaka 2024 kutimiza azma ya Serikali ya kuhakikisha huduma ya majisafi maeneo ya mijini inafikia asilimia 95 au zaidi ifikapo 2025.

    Aidha Mha.Katakweba amewaahidi ushirikiano wa dhati katika kila hatua ya utekelezaji wa mradi huo.

    Kwa upande wake Meneja Mradi kutoka Kampuni ya Egis Water and Martime Mha. Hudhaifa Hajj ameahidi kutekeleza Mradi kwa wakati na kwa kuzingatia ubora. Mradi wa uboreshaji huduma ya majisafi na usafi wa mazingira Morogoro unafadhiliwa na Serikali kupitia mkopo wenye masharti mafuu kutoka Shirika la maendeleo Ufaransa ba utagharimu zaidi ya Tsh. Bilioni 185 za kitanzania.

    Posted On : september, 25,2023

  • MORUWASA, WAMIRUVU KUSHIRIKIANA NA WORLD WATERNET KUHIFADHI KIDAKIO CHA NGERENGERE.

    Shirika la World Waternet Kupitia Progamu ya WaterWorx limekutana na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) na Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu na kujadili mpango kazi wa pamoja wa kuhifadhi kidakio cha Ngerengere katika kikao kilichofanyika mapema leo Agosti,25,2023 katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa MORUWASA

    .

    Mpango kazi huo ambao unalenga kurejesha uoto katika kidakio na hifadhi ya Bwawa la Mindu unahusisha uandaaji wa mfumo wa kufanya maamuzi ili kuchagua aina ya kilimomsitu kwa kuzingatia faida za kiuchumi kwa jamii inayoishi pembezoni mwa vyanzo vya maji na faida za kimazingira.

    aasisi za TAFORI na Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) pia zimeshiriki katika kikao hicho wakiwa ni wadau muhimu wa kuhifadhi mazingira katika kidakio cha Ngerengere na hifadhi ya  Bwawa la Mindu.

    Posted On : Ugust, 25,2023

  • MORUWASA YASHIRIKISHA WADAU MAPENDEKEZO YA BEI MPYA ZA MAJI

    Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) imekutana na wadau mbalimbali na kupokea maoni yao kuhusu mapendekezo ya bei Mpya za huduma za Maji kwenye kikao kilichofanyika leo Agosti 24,2023 katika ukumbi wa Hoteli ya Edema, Morogoro.

    Wadau mbalimbali kutoka maeneo yanayohudumiwa na MORUWASA ya Manispaa ya Morogoro, Miji ya Kilosa na Mikumi na maeneo ya Mkambarani, Dakawa, Dumila na Mzumbe wameweza kuwasilisha maoni yao kuhusu mapendekezo ya Bei Mpya yaliyowasilishwa na MORUWASA.

    Awali akifungua kikao hicho, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mjini Mhe. Rebeca Nsemwa ameipongeza MORUWASA kwa hatua ya kushirikisha wadau na kuwataka wajumbe hao kuzingatia maslahi mapana ya wananchi katika maoni yao.

    Wadau mbalimbali walioshiriki kikao hicho ni pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Ofisi ya Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro na viongozi wa Wilaya za Morogoro Mjini, Morogoro DC , Mvomero na Kilosa.

    Wengine ni Viongozi wa Dini Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na vyama vya upinzani, Waandishi wa Habari , Taasisi za Umma na wawakilishi wa wananchi Viwanda, Vyuo, Hoteli na wawakilishi wa mwananchi mmoja mmoja.

    Maoni yaliyotolewa na wadau yatazingatiwa katika uboreshaji wa huduma na yatawasilishwa kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kuidhinisha bei mpya za huduma za maji zitakazotumika mpaka 2025/2026.

    Posted On : August,24,2023.

  • MHE. JAFO AIPA HEKO MORUWASA

    Baadhi ya watumishi wakiwa pamoja katika zoezi la ufuatiliaji bili za maji kwa watejaWaziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Dkt. Selemani Jafo amepongeza jitihada zinazofanywa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) katika kuhakikisha inamtua mama ndoo kichwani.

    Mhe. Jafo, ametoa pongezi hizo leo Agosti 7,2023 alipotembelea Banda la MORUWASA kwenye maonesho ya Nanenane kanda ya Mashariki yanayoendelea katika viwanja vya J.K. Nyerere mkoani Morogoro.

    Aidha, ameitaka MORUWASA kuendelea kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na elimu ya kuzuia shughuli za kibinadamu zinazofanyika pembezoni mwa vyanzo vya maji ili kuepusha kujaa kwa tope katika Bwawa la mindu ambalo ni chanzo mama cha maji kwa wakazi wa Morogoro. Sambamba na hilo amesisitiza juu ya utoaji wa elimu kuhusu athari ya vitendo vya uchomaji moto wa misitu iliyopo katika Milima ya Uluguru ili kuhifadhi mazingira na vyanzo maji.

    MORUWASA inashiriki maonesho ya nanenane huku ikisogeza karibu huduma mbalimbali zinazotolewa na Mamlaka hiyo pamoja na utoaji wa elimu ya umuhimu wa utunzaji wa Mazingira na vyanzo vya maji kwa wananchi wanaojitokeza katika maonesho hayo.

    Posted On : August,7,2023

  • Ziara ya katibu mkuu wizara ya maji

    Katibu mkuu akiwa na badhi ya watendaji wa MORUWASA wakati wa ziara yake alipotembele maeneo tafauti kuangalia miradi ya maji inayo endelea

    Posted On : .....